Habari za michezo

BAADA YA ‘KUIBANJUA KIMOKO’ NAMUNGO…MGUNDA AFUNGUKA YA MOYONI SIMBA..

admin November 17, 2022 4:00 pm

Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo FC umempa nafasi Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Ramadhana Mgunda, kuwashukuru Wachezaji wake kwa kazi kubwa walioifanya jana Jumatano (Novemba 16), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Bao la ushindi la Simba SC lilipachikwa wavuni na Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Moses Phiri dakika 31, na kuifanya klabu hiyo kufikisha alaama 24 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mgunda amesema wachezaji wake walipambana na kuonesha njaa ya kusaka ushindi kwenye mchezo huo, ambao amekiri ulikua mgumu kutokana na Wapinzani wao kuwa na uwezo wa kupambana na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

“Wachezaji wangu wameonesha kupambana na ndio maana tumefanikiwa kupata alama tatu kwenye mchezo huu, ninaamini walidhamiria kufanya hili tulilipata,”

“Hata wapinzani wetu walifanya kazi kubwa sana kwa kucheza soka lililotupa changamoto wakati wote, walikua shap katika kushambulia kila walipopata nafasi, ila wachezaji wangu walionesha kuwa makini na kuzima kilichokusudiwa dhidi yetu.” amesema Mgunda.

Simba SC itarejea tena Dimbani Jumamosi (Novemba 19) kucheza dhidi ya Ruvu Shooting itakayokua nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

UKWELI MCHUNGU…SIMBA SC WASIPOJIANGALIA KATIKA HAYA…HATA HUKO KIMATAIFA WASAHAU… KISA KOCHA KUKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA…WADAU WAMKALIA KOONI MANGUNGU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply