Azam FC

PAMOJA NA KUISHINDISHA AZAM…ONGALA ASHINDWA KUJIZUIA…AFUNGUKA ANAVYOTESEKA…

admin December 1, 2022 5:49 am

Kali Ongala, Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara ni mgumu kwa kuwa kila timu inahitaji pointi tatu.

Ongala amekuwa kwenye mwendo bora na kikosi cha Azam FC ambapo mchezo wake wa kwanza aliwatungua Simba bao 1-0 Uwanja wa Mkapa na mtupiaji alikuwa ni Prince Dube.

Ushindi mkubwa ambao ameupata akiwa kwenye benchi la ufundi ni ule wa Mtibwa Sugar 3-4 Azam FC kwenye mchezo wa kukata na shoka uliochezwa Uwanja wa Manungu.

Mchezo wake uliopita alishuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Azam FC 3-2 Coastal Union na mchezo huo wachezaji wa Coastal Union walionekana kuleta vurugu kwa mwamuzi pengine labda ni kutokana na maamuzi yake kwenye mchezo huo jambo ambalo linafuatiliwa na kamati kwa sasa.

Ongala amesema:”Kila mchezo ni mgumu na wapinzani wanafanya kazi kubwa kusaka matokeo, kikubwa ni kuona tunashinda na kupata pointi tatu,”.

Azam FC imekusanya pointi 32 baada ya kucheza mechi 14 kwenye msimamo ipo nafasi ya pili.

TULIENI SASA….WINGA MUIVORY COAST KUTUA SIMBA SC…KISA KIPIGO…NABI AWAJAZA UPEPO MASTAA YANGA… BAADA YA ‘KUTOBOLEWA JUZI’…YANGA SASA WAPUMUA…’PRESHA’ YA ‘UNBEATEAN’ ILIWANYIMA RAHA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply