Habari za michezo

TZ PRISONS KULAMBA MILIONI 20 CASH WAKIIFUNGA YANGA JUMAPILI HII….

admin December 2, 2022 7:57 am

Wadhamini wa ‘wajelajela’ Tanzania Prisons ya Mbeya, Silent Ocean, wametoa ahadi ya milioni 20 kwa wachezaji wa timu hiyo ikiwa watafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Yanga SC katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara siku ya Jumapili tarehe 4 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Tanzania Prisons waliopo nafasi ya 11 wakiwa na point 15 baada ya kucheza mechi 14 ikiwa wataifunga Yanga watakuwa wametia chumvi kidonda kwa kuwafanya mabingwa hao wa kihistoria kuchezea vipigo viwili mfululizo baada ya kipigo cha kwanza cha 2-1 walichokipata siku ya jana toka kwa Ihefu SC ambayo imeikomesha rekodi ya Yanga ya kutofungwa mechi 49 mfululizo.

Wajelajela hao hawataondoka mikono mitupu pia ikiwa watafanikiwa kupata sare dhidi ya Yanga kwa kuwa mdhamini wao, Silent Ocean, amewawekea kitita cha milioni kumi kwa matokeo ya sare ya aina yeyote.

NABI : HAWA SIMBA WATAANZA KUSHINDA MECHI ZAO KWA KASI… MGUNDA : YANGA KUFUNGWA KUMETUAMSHIA ARI YA UBINGWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply