Tetesi za Usajili Yanga
Habari za michezo

MAYELE PAMOJA NA MASTAA HAWA WA YANGA KUKOSEKANA KESHO DHIDI YA TZ PRISONS…

admin December 3, 2022 7:19 pm

KUELEKEA kwenye mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons kuna baadhi ya nyota wa Yanga ambao wataukosa mchezo huo.

Kwa mujibu wa Cedrick Kaze, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa wapo ambao wataukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali.

“Dickson Job ana adhabu hatakuwepo kwenye mchezo wa kesho, Jesus Moloko na Mayele hawajafanya mazoezi tutawaangalia kwenye mazoezi ya leo kama watatumika kwenye mchezo wa kesho.

“Bernard Morrison na Bakari Mwamnyeto wamerudi mazoezini lakini bado hawako vizuri asilimia mia moja,”.

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza mechi 13 mchezo wake uliopita ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu ya Mbeya.

FT:COASTAL UNION 0- 3 SIMBA SC…MOSES PHIRI KAMA MAYELE TU….CHAMA AZIDI KUSAMBAZA UPENDO… MAAJABU YA MIPIRA KOMBE LA DUNIA…HUWA INACHAJIWA KAMA SIMU KABLA YA MECHI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply