Habari za michezo

BALAA…MANZOKI AIWEKA SIMBA SC ROHO JUU…DILI LAKE LINAUKAKASI…

admin December 25, 2022 7:09 am

WAKATI matumaini makubwa ya kumalizana na mshambuliaji wa Dalian Profesional ya China, taarifa zinasema ameumia na inatakiwa afanyiwe upasuaji.

Taarifa za uhakika kutoka jijini Beijing, China zinasema hadi jana, Manzoki alikuwa amekosa mechi sita za kikosi chake baada ya kuumia.

“Aliumia katika mechi ya michuano ya Kombe la FA hapa, alikuwa anaingia na mpira baada ya kumtoka beki, mwingine akamkwatua ndani ya eneo la 18.

“Bahati mbaya Dallian hata hiyo penalti hawakupewa, si unajua huku kuna hayo mambo ya kamari, wakati mwingine yanaharibu sana mpira,” kilieleza chanzo.

“Manzoki alikuwa tegemeo kwenye kikosi cha Dallian na mkataba wake ulikuwa unaisha mwisho wa hii Desemba.”

Taarifa nyingine zimeeleza kuwa Manzoki raia wa Afrika ya Kati, amekataa katakata kufanya upasuaji nchini China akisisitiza atatibiwa barani Afrika.

Juhudi za kumpata Manzoki bado hazijafanikiwa lakini hofu kwa Simba SC kama itaweza kumsajili mchezaji aliyeumia.

Simba SC ilikuwa imeweka uhakika wa kumsajili Manzoki kutokana na kutokuwa na mshambuliaji hatari wa kati baada ya kuondoka kwa Dejan Georgijević.

Bado viongozi wa Simba SC hawajesema lolote kuhusiana na Manzoki ambaye amekuwa midomoni mwa Wanasimba tangu ilipoelezwa atajiunga na kikosi chao wakati wa dirisha kubwa la usajili.

Dalili zinaonyesha Simba SC watalazimika kutafuta mshambulizi mwingine na si Manzoki kwa kuwa kama kuumia kwake kunamlazimisha kufanya upasuaji, maana yake atakuwa nje kwa zaidi ya miezi miwili.

YANGA WAMGOMEA FEI TOTO…AZAM WAMFUATA MAMA YAKE…INONGA ANAFUATA…. MIL 350 KUMSHUSHA PACHA WA PHIRI SIMBA SC….JAMAA LINAJUA HILOO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply