Home Habari za michezo MKUDE AVUNJA UKIMYA SIMBA SC…AFUNGUKA A-Z KILICHONYUMA YA PAZIA..

MKUDE AVUNJA UKIMYA SIMBA SC…AFUNGUKA A-Z KILICHONYUMA YA PAZIA..

Habari za Simba leo

Kiungo Jonas Mkude hajaonekana kwa muda uwanjani, huku ikielezwa pia mkataba wake upo ukingoni kabla ya kumalizika na kuleta hofu kwa mashabiki na wanachama wa Simba, lakini mwenyewe amevunja ukimya na kuwatuliza akiwaambia bado yupo sana Msimbazi.

Mkude amekuwa hana nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha Juma Mgunda, lakini  alisema kutoonekana kwake uwanjani kumetokana na kuwa majeruhi na hata alivyorudi hakuwa fiti kivile, tofauti na wachezaji waliochukua nafasi yake kikosini.

Kiungo huyo mkabaji ambaye ni mwandamizi kwenye kikosi cha sasa cha timu hiyo, alisema kwa sasa yupo fiti tayari kuliamsha kikosini na kufichua ishu ya mkataba wake alisema wanapaswa kuulizwa na viongozi wa timu.

“Kuna muda nilipata majeraha, sikuweza kufanya mazoezi na timu na hata nilivyopona ilihitaji muda pia ili kurudi kwenye utimamu kama wenzangu ndio maana mara nyingi nilikuwa sionekani uwanjani na muda mwingine naanzia benchi,” alisema Mkude na kuongeza;

“Kwa sasa niko poa na tayari kwa mapambano nadhani kilichobaki ni kwa benchi la ufundi kuamua kunitumia.”

Kocha Mgunda alisema Mkude ni mchezaji mzuri na yupo Simba ili kuhakikisha inatimiza malengo hivyo yupo kwenye mipango yake na atamtumia kutokana na matakwa ya mchezo husika.

“Ni mchezaji mwenye uzoefu wa kutosha, anastahili kuichezea Simba na nitamtumia kutokana na uhitaji wa mechi kwani yupo hapa ili kuitumikia timu,” alisema Mgunda, huku ikielezwa Mkude ni kati ya wachezaji wa Simba ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu na hadi sasa ikielezwa hakuna mazungumzo yaliyoanza kwa ajili ya kuongezwa mpya.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here