Habari za michezo

WAKATI KOMBE LA DUNIA LIKIENDELEA…WAARABU WAZIRUDISHA ARSENAL NA LIVER UWANJANI …

admin December 5, 2022 4:00 pm

Vinara wa Ligi Kuu ya England ‘Arsenal’ watarejea tena Uwanjani baadae juma ili, huku Fainali za Kombe Dunia zikiendelea kurindima nchini Qatar.

Arsenal itapasha misuli joto kabla ya kuendelea kwa Mshike Mshike wa Ligi Kuu ya England kwa kucheza Michuano maalum ‘Dubai Super Cup’ itakayoshirikisha timu nyingine tatu za Barani Ulaya.

Klabu ya Olimpic Lyon ya Ufaransa, AC Milan ya Italia, Arsenal na Liverpool zote za England zimealikwa kwenye Michuano hiyo ambayo rasmi itaanza siku ya Alhamis (Desemba 08) Dubai.

Hata hivyo katika Michuano hiyo timu za England (Arsenal na Liverpool) hazitakutana, na badala yake zitacheza dhidi ya timu nyingine shiriki kutoka Italia na Ufaransa.

Kwa sasa Ligi Kuu za Mataifa ya Ulaya zimesisimama kupisha Fainali za Kombe la Dunia, zitakazofikia tamati Desemba 18, huko nchini Qatar.

TETESI:….MASTAA HAWA WATANO ‘KULIWA VICHWA’ SIMBA SC…AKPAN APATA PAKUHEMEA… ILE ISHU YA AUCHO KUOMBA KUSEPA YANGA…KUMBE UKWELI UKO HIVI ‘BANA’…FEI TOTO ATAKA MSHAHARA WA MAYELE..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply