Habari za Simba SC
Habari za michezo

KUHUSU KUMSAJILI BOBOSI…SIMBA SC WAPIGILIA MSUMARI….DILUNGA ATAJWA…

admin January 6, 2023 2:27 pm

Meneja wa Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amefunguka na kusema kuwa katika dirisha hili dogo la usajili hawana mpango wa kumsajili aliyekua kiungo wa Klabu ya Vipers, Bobosi Byaruhanga.

Ally alifunguka: ” Tunatarajia kuongea nguvu katika eneo la kiungo mkabaji ambaye atatusaidia kutimiza malengo yetu msimu huu.

“Hatuwezi kumsajili Bobosi kwasababu tayari alishawahi kushiriki michuano ya kimataifa msimu huu, hivyo hatoweza kuwa na mchango wowote katika michuano yetu ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tunahitaji mchezaji ambae tutaweza kumtumia katika michuano au mashindano yote tunayoshiriki ndani na nje ya nchi.

“Kumsajili Bobosi itakua ni kama tumemsajili kwa ajili ya kucheza mechi kumi za Ligi Kuu Bara zilizobaki tu jambo ambalo hatuwezi kufanya.

“Bobosi ni mchezaji kijana mwenye viwango na ubora wa hali ya juu, lakini msimu huu hatuwezi kumsajili.”

Ukiacha Bobosi, Simba SC pia imehusishwa kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya Vipers Manzoki ambaye anakipiga nchini China kwa sasa.

Katika dirisha hili dogo la usajili, tayari Simba SC imeshamsajili Saido Ntibazonkiza kutoka Geita gold, huku ikitajwa pia iko mbioni kumrudisha kundini Hassan Dilunga ambaye aliachwa kutokana na kuwa majeruhi.

HAJI MWINYI.: YANGA SC BADO HAIJAPATA BEKI KAMA MIMI….WALINIFANYA NIKAPOTEZA ‘DEMU’… KUHUSU HATMA YA KINA KIBU NA OKWA…SIMBA SC WAMPA MUDA KOCHA MBRAZILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply