Nelson Okwa akiwa Simba SC
Habari za michezo

BAADA YA KUPELEKWA IHEFU DK ZA JIONI…OKWA ASHINDWA KUJIZUIA…AFUNGUKA MAPYA KWA SIMBA…

admin January 17, 2023 6:39 pm

Kiungo kutoka nchini Nigeria Nelson Esor Okwa kwa mara ya kwanza amefunguka, baada ya kuondoka kwa mkopo Simba SC na kutimkia Ihefu FC.

Kiungo huyo ambaye alisajiliwa Simba SC mwanzoni mwa msimu huu akitokea Rivers United ya kwao Nigeria, amelazimika kuondoka klabuni hapo kwa mkopo baada ya kushindwa kufikiwa kiwango cha kuingia kwenye kikosi cha kwanza.

Okwa amesema yupo tayari kucheza Ihefu FC na ndio maana amekubali kujiunga nayo, huku akiamini anaweza kurejea Simba SC mwishoni mwa msimu huu akiwa na kiwango bora, kitakachomuwezesha kucheza kikosi cha kwanza.

Amesema kuhusu mazingira mapya aliyoyakuta Ihefu FC ni tofauti na Simba SC, lakini bado akasisitiza kupambana na kufanikisha mpango wa kurudi katika kiwango chake.

“Suala kubwa hapa ni kupambana katika klabu yangu mpya, nitahakikisha ninacheza kwa kiwango cha juu ili niweze kurudi Simba SC nikiwa vizuri na kuingia kwenye kikosi cha kwanza.”

“Mazingira hayawezi kufanana, lakini kilichonileta huku ni kucheza soka, kwa hiyo kazi kubwa iliyonileta Ihefu FC nitahakikisha naipambania ili kufanikisha kusudio la kurudisha kiwango changu.” amesema Nelson Okwa

Hadi anaondoka Simba SC kwa mkopo, Okwa alikuwa ameshacheza michezo mitatu ya Ligi Kuu pamoja na mchezo mmoja wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

WAZUNGU WAJITOSA KUIOKOA GEITA GOLD…ISHU NZIMA IKO HIVI…. BIGIRIMANA AWASHA MOTO YANGA…ATAKA ALIPWE CHAKE ASEPE….MABOSI WAMUOMBA POO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply