Bigirimana akiwa Yanga SC
Habari za michezo

BIGIRIMANA AWASHA MOTO YANGA…ATAKA ALIPWE CHAKE ASEPE….MABOSI WAMUOMBA POO…

admin January 17, 2023 8:33 pm

Yanga ilifunga usajili kwa kumtambulisha Mamadou Doumbia huku usajili huo ukitajwa kumng’oa kiungo Gael Bigirimana.

Gael Bigirimana amesajiliwa na Yanga msimu huu lakini ameshindwa kujihakikishia namba ya kudumu katika kikosi cha Wananchi.

Inaelezwa Gael amehitaji malipo yote ya kuvunja Mkataba na mengine ya nyuma ili akasake riziki kwingine huku Uongozi wa Yanga ukiomba kulipa kidogo kidogo.

Wanancho wanahitaji kupunguza baadhi ya wachezaji wa kigeni ili wabaki 12 wanaoruhusiwa kwa kanuni za TFF.

Mbali na hivyo, mabosi wa Jangwani wanaangalia uwezekano wa kupunguza gharama za kuhudumia wachezaji haswa kwenye upande wa mishara, hali iliyopelekea kuachana pia na Yacouba Sogne ambaye amejiunga na Ihefu,huku Lazaro Kambole akirudi zake Zambia kujiunga na Zesco.

Pamoja na Gael, Tuisilia Kisinda naye anatajwa kuwa kwenye mpango huo,japo kwa upande wake hakuna presha sana kutokana na kwamba yeye anaichezea Yanga kwa Mkopo akitokea Berkane ya Morocco.

BAADA YA KUPELEKWA IHEFU DK ZA JIONI…OKWA ASHINDWA KUJIZUIA…AFUNGUKA MAPYA KWA SIMBA… KAMBI YA SIMBA DUBAI YAJIBU….AHMED ALLY AFUNGUKA WALICHOPEWA NA CSKA MOSCOW…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply