Habari za Yanga
Habari za michezo

AUCHO NI MAJANGA JUU YA MAJANGA YANGA….ISHU NZIMA IKO HIVI…

admin January 19, 2023 2:31 pm

Klabu ya Yanga imetoa taarifa kuwa kiungo wake Khalid Aucho raia wa Uganda amepata jeraha la mguu wake wa kushoto na atakuwa nje kwa kipindi cha wiki moja.

Taarifa hiyo inakuja kufuatia tetesi kusambaa zikidai kuwa Mganda huyo amegomea kujiunga na timu kwa kile kinachodaiwa kuwa anataka alipwe pesa zake za kusaini mkataba ndani ya klabu hiyo ambao alisaini hivi karibuni ambazo hajalipwa.

Kwa mujibu wa vipimo vilivyosimamiwa na daktari wa Yanga, Moses Etutu, Aucho hajavunjika bali ni mshipa wa mguu umevimba baada ya mshituko alioupata akiwa mazoezini.

“Mwanzo tulidhani shida ni kubwa kidogo lakini baada ya vipimo tumegundua hajavunjika bali mshipa tu umevimba, atakuwa nje ya uwanja kwa wiki moja tu,” alisema Daktari.

WAGOMBEA SIMBA WALIA NA KATIBA KUMBEBA MWEKEZAJI….WAAPA MABADILIKO… HIZI HAPA SABABU YA KIFO CHA MCHEZAJI WA U17 WA SINGIDA BIG STAR ALIYEFIA UWANJANI LEO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply