Habari za Simba SC
Habari za michezo

ISHU YA ‘SUB’ YA CHAMA…MGUNDA NAYE ASHINDWA KUJIZUIA…AIBUKA NA HILI KUHUSU MBRAZILI…

admin January 20, 2023 7:25 pm

Kocha Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kumpa muda kocha wao Roberto Oliveira ‘Robertinho’, ili aweze kujenga timu imara ya mataji.

Kocha huyo ameeleza kuwa kitendo cha kuanza kumkosoa ikiwa ndio kwanza ameanza kufanya majukumu yake ni kumfanya aone ugumu katika kazi yake mpya.

“Robertinho ni kocha mzuri ameonesha hivyo tangu akiwa Uganda, hivyo tunapaswa kumpa muda ukizingatia amekuja kwenye timu mpya na mazingira ni tofauti na alikotoka tunapaswa kumpa muda,” amesema Mgunda.

Baadhi ya mashabiki wa Simba, walionesha kutofurahishwa na kocha huyo baada ya kumfanyia mabadiliko kiungo mchezeshaji wa timu hiyo Clatous Chama kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City ambao ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 3-2.

BAADA YA KUWA ‘CHIMBO’ KWA MUDA MREFU…MORRISON NA AZIZI KI WAJITOKEZA YANGA… KUHUSU BALEKE KUSAJILIWA KWA MKOPO…BOSI SIMBA AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA MKATABA ULIVYO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply