Habari za Simba
Habari za michezo

KUHUSU BALEKE KUSAJILIWA KWA MKOPO…BOSI SIMBA AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA MKATABA ULIVYO…

admin January 20, 2023 7:30 pm

Baada ya kuenea kwa taarifa kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Simba, Jean Baleke kwamba ametua hapo kwa mkopo akitokea TP Mazembe, uongozi  umeibuka na kutoa ufafanuzi.

Baleke raia wa DR Congo, amejiunga na wekundu wa msimbazi katika usajili wa dirisha dogo uliofungwa Januari 15, mwaka huu.

Meneja wa Habari na mawasiliano wa Mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu, Ahmed Ally, alifunguka kuwa: “Tetesi au maneno yanayoendelea kuhusu mkataba wetu na Jean Baleke kuwa tumemchukua kwa mkopo sio za kweli.

“Baleke tumemsajili katika dirisha dogo la usajili kwa kandarasi ya miaka miwili kutoka TP Mazembe, kwa hiyo tutakuwa na Belake mpaka 2025.

“Eneo la straika lilikuwa na nafasi moja ya wazi, kwa hiyo tusingeweza kujaza nafasi hiyo kwa kumchukua mchezaji kwa mkopo, Simba hatuna tamaduni hiyo na malengo yetu hayaendani na taratibu hizo.”

ISHU YA ‘SUB’ YA CHAMA…MGUNDA NAYE ASHINDWA KUJIZUIA…AIBUKA NA HILI KUHUSU MBRAZILI… KAMA ZALI AISEE…TIMU ZA MBEYA ZILIVYOMRUDISHA MJINI NTIBAZONKIZA….ISHU NZIMA IKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply