Habari za Simba SC
Habari za michezo

PAMOJA NA UWEPO WA MBRAZILI…MGUNDA AWATEGA MASTAA SIMBA MECHI YA LEO…

admin January 22, 2023 6:45 am

Kocha msaidizi wa klabu ya Simba, Juma Mgunda amesema kwa sasa wanawaza mchezo unaofuata wa leo dhidi ya Dodoma Jiji ili waweze kupata matokeo mazuri, huku akiahidi boli litatembea sana tu kwenye Uwanja wa Jamhuri, utakaotumika kwa mchezo huo wa Ligi Kuu Bara.

Simba juzi Januari 20, 2023 ilitua makao makuu ya nchi kukipiga dhidi ya Dodoma Jiji kesho ikiwa imetoka kuifunga Mbeya City kwa mabao 3-2 juzi, huku wenyeji wakitoka kulala ugenini kwa mabao 2-0 mbele ya Geita Gold, mjini Geita na Mgunda aliyeisambaratisha Dodoma kwa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza alisema jana jioni kikosi kilirejea kuendelea na maandalizi ya mchezo huo wakipania kuendeleza ubabe.

Mgunda alisema benchi la ufundi kwa kushirikiana na wachezaji wanapambana kuhakikisha Wanasimba wanafurahia kila mchezo ambao timu yao itacheza.

“Sisi walimu tunafanya majukumu yetu, lakini dakika 90 tutawaachia wachezaji kuhakikisha wanazitumia vyema kupata matokeo,” alisema Mgunda ambaye alikuwa kocha mkuu wa Simba kabla ya Mbrazili Roberto Oliveira ‘Robertinho’ kuja.

ISHU YA KUFANYIWA ‘SUB’ SIMBA….CHAMA KWA MARA YA KWANZA AIBUKA NA MSIMAMO HUU.. YANGA WAIBUKA NA ISHU YA PSG KUWAIGA KWENYE JEZI….MADAI YAO YAKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply