Habari za Michezo Bongo
Habari za michezo

KUTOKA KAMBI YA YANGA….KAZE AVUNJA UKIMYA …AFUNGUKA KUHUSU DHARAU ZA MASTAA…

admin January 28, 2023 2:07 pm

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amewataka wachezaji wake kutozidharau timu ambazo wamepangwa nazo kwenye hatua za awali za Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Kocha huyo ameeleza kuwa wachezaji wengi wakubwa wamekuwa hawapendi kucheza mechi hizo na hata wakicheza hawajitoi kama wanapokutana na timu nyingine kwenye ligi.

“Wachezaji watambue haya ni mashindano ya mtoano, ili ufike fainali ni lazima uifunge kila timu unayokutana nayo bila kujali ukubwa wake, hivyo kudharau timu ndogo kunaweza kufifisha malengo tuliyokusudia kuyafikia msimu huu,” amesema Kaze.

Yanga kesho Jumapili watacheza na Rhino Rangers ya Tabora huo ukiwa ni mchezo wa raundi ya tatu wa michuano hiyo ambayo miamba hiyo ndio mabingwa watetezi.

FANYA JUU CHINI KUHAKIKISHA MKEKA WAKO WA MERIDIANBET UNA ODDS HIZI ZA UHAKIKA… HUYU NDIYE NABI MZEE WA MAREKODI…REKODI HII NYINGINE MPYA KAWEKA NA YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply