Kocha Msaidizi Simba SC
Habari za michezo

SIKU CHACHE BAADA YA MBRAZILI KUSEPA…MGUNDA ASHUSHA PRESHA SIMBA…

admin January 28, 2023 2:23 pm

Kocha Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amewataka mashabiki wa timu hiyo kutulia kwa kuwa mikakati yao ya kutaka kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara bado haijapoteza mwelekeo kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo.

Mgunda ametoa kauli hiyo wakati Simba ikiwa inakabiliwa na mchezo wa Kombe FA dhidi ya Coastal Union leo Jumamosi kabla ya kucheza na Singinda Big Stars, Februari 3, mwaka huu kisha kucheza mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Horoya Februari 10, mwaka huu.

Mgunda amesema kuwa, wanatambua ugumu wa michuano iliyo mbele yao lakini ni wakati wa mashabiki wa timu hiyo kutulia na kuweza kuwaunga mkono ili waweze kufikia malengo waliojiwekea msimu huu kwenye michuano yote.

“Nadhani ni wakati wa mashabiki kuweza kutupa sapoti kubwa ya kuhakikisha tunaendelea kupambana kulingana na mechi ambazo zipo mbele yetu ili kuweza kufikia malengo ya timu kutokana na kile ambacho tunahitaji kuweza kukipata kutoka katika kila mchezo.

“Ukiangalia ligi bado ngumu na inakuwa na ushindani mkubwa kutokana na wapinzani wetu kujipanga vizuri lakini tumekuwa katika nafasi ya kuanza kampeni ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu tunataka kuona kila mchezo tunaweza kushinda kutokana sapoti kubwa ambayo tunaweza kuipata kutoka upande wao,” alisema Mgunda.

HUYU NDIYE NABI MZEE WA MAREKODI…REKODI HII NYINGINE MPYA KAWEKA NA YANGA… SAKHO AZALIWA UPYA SIMBA….KWA HILI ANALIFANYA ‘HUYU DOGO’..YANGA MSAHAU UBINGWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply