Habari za Yanga
Habari za michezo

HUU HAPA UKWELI KUHUSU MORRISON KUONDOLEWA YANGA…ISHU NZIMA IKO HIVI…

admin February 5, 2023 1:59 pm

Daktari wa timu ya Yanga, Moses Etutu ametoa taarifa ya maendeleo ya wachezaji wetu wawili Abutwalib Mshery pamoja na Bernard Morrison ambao wapo nje ya kikosi hicho wakiuguza majeraha tofauti.

Akizungumza na YANGA MEDIA, Daktari Moses alisema kuwa kipa wao, Abutwalib Mshery atakuwa nje kwa takribani miezi 3-4.

“Mshery ana tatizo la goti kitaalamu inaitwa “meniscus grade 2 tear” ambapo ataenda kufanyiwa upasuaji nchini Tunisia na baada ya hapo atarejea kwa ajili ya uangalizi wa karibu,” amesema Dk. Etutu.

Kwa upande mwingine, Dk. Etutu pia amezungumzia kuhusu mchezaji Bernard Morrison ambae nae yupo nje kwa muda mrefu.

“Morrison ana tatizo la nyama za paja (pubalgia) na atakuwa nje kwa muda wa miezi miwili, na ameshaanza kutibiwa mpaka sasa akiwa ameshakamilisha asilimia 40% ya matibabu yake,” amesema Dkt. Etutu.

Aidha, Morrison anatibiwa na ataendelea kutibiwa hapa hapa nchini Tanzania kwani tatizo lake ni kawaida na linawezekana kutibiwa nchini bila kwenda nje ya nchi.

ACHANA NA ‘ASISTI’ ZA CHAMA…HIVI NDIVYO SAIDO ANAVYOWANYANYASA WOTE LIGI KUU… CHAMA AINGIA KWENYE MFUMO WA MBRAZILI…SIRI HII YAANIKWA…AZIZ KI AMVIMBISHA KICHWA NABI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply