Habari za Yanga
Habari za michezo

KUTOKA TUNISIA…YANGA ‘WAJIWEKA MGUU SAWA’…KAZE AVUNJA UKIMYA HALI ILIVYO…

admin February 10, 2023 4:02 pm

Kikosi cha Yanga kimefanya mazoezi ya kwanza ya ufundi asubuhi ya jana kwenye viwanja vya Olympic de Rades nchini Tunis, Tunisia kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir ya nchini humo.

Mazoezi haya yaliodumu kwa saa moja na nusu yalianza saa 10:30 kwa saa za Tunisia [Sawa na saa 12:30 mchana kwa Tanzania].

Akizungumza na Yanga Media kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze alisema, wao kama benchi la ufundi wanafurahishwa na maandalizi mazuri yaliyofanywa na uongozi wa Yanga kuelekea mchezo wa Jumapili, dhidi ya Monastir ya Tunisia.

“Leo (jana) tumefanya mazoezi ya pili hapa Tunisia, jana tulianza na recovery na leo tumekuja uwanjani. Kila kitu mpaka sasa kiko sawa na wachezaji wanaonyesha kuwa na furaha na kujituma sana,” alisema Kaze.

Wachezaji wote 24 walihudhuria mazoezi haya yaliyosimamiwa na kocha mkuu, Nasredine Nabi kasoro golikipa Aboutwaleb Mshery aliyesafiri kwenda Sousse kwa ajili ya matibabu.

KUELEKEA MECHI YA KESHO DHIDI YA HOROYA…MANULA ‘ACHANWA LIVE’ KUHUSU UDHAIFU WAKE… KISA TUHUMA ZA USHIRIKINA…MBRAZILI AINGILIA KATI BIFU LA KAPOMBE NA MWENDA…ISHU NZIMA IKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply