Mashabiki wa Yanga
Habari za michezo

BAADA YA KUWAKUNG’UTA MAZEMBE JANA…YANGA WATOA TAARIFA HII MPYA KWA MASHABIKI…

admin February 20, 2023 12:04 pm

Uongozi wa Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga SC umewashukuru Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kwa ushirikiano waliouonesha Kabla, Wakati na Baada ya mchezo wa Mzunguuko wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Yanga SC iliikaribisha TP Mazembe ya DR Congo, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam jana Jumapili (Februari 19) na kupata ushindi wa 3-1.

Shukran kwa Wanachama na Mashabiki wa Yanga SC zimetolewa na Uongozi wa Klabu hiyo kupitia kurasa za Kijamii za Klabu hiyo, huku ukiwasisitiza kuendelea kuwa bega kwa bega na timu yao katika kipindi hiki cha kusaka nafasi ya kufuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Taarifa ya Uongozi wa Yanga  iliyochapishwa kwenye Kurasa za Mitandao ya Kijamii: “Shukrani kwa Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Young Africans SC kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wetu wa kimataifa dhidi ya TP Mazembe kwenye Dimba la Benjamin Mkapa jana.

Hakika ushindi wa jana ni Heshima kwetu, Klabu yetu na Taifa kwa ujumla.”

Yanga itacheza mchezo wa Mzunguuko wa Tatu wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika Jumapili (Februari 26) dhidi ya Real Bamako ya Mali.

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam kuelekea Bamako-Mali, baada ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC FC utakaopigwa keshokutwa Jumatano (Februari 22).

PAMOJA NA KUFUNGWA JUZI…KUMBE MO DEWJI ALISHAWAPA ‘MAKAVU’ MASTAA WOTE WA SIMBA … KIPIGO CHA SIMBA CHAMFANYA AHMED ALLY KUFUNGUKA YA MOYONI…ADAI KUNA NAMNA ….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply