Habari za Simba
Habari za michezo

AHMED ALLY: VIPERS WATAJUTA KUJA KUCHEZA NA SIMBA DAR…..MOTO UTAWAHUSU…

admin March 7, 2023 9:58 am

Uongozi wa Klabu ya Simba SC umeweka wazi kuwa mara baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza wakiwa nyumbani katika Uwanja wa Mkapa dhidi ya Raja Casablanca, safari hii hawataki utani watakapokutana na Vipers SC wakiwa nyumbani katika uwanja huo huku wakisema kuwa timu hiyo wataipelekea pumzi ya moto.

Simba SC katika mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco walipoteza kwa kufungwa mabao 3-0, mchezo wao wapili wakiwa nyumbani wanatarajiwa kucheza kesho Jumanne dhidi ya Vipers.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed amesema wamejifunza kutokana na makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo huo, na sasa wamejipanga kushinda katika Uwanja wa nyumbani dhidi ya Vipers SC.

“Mchezo wa kwanza ni kweli tulipoteza tukiwa nyumbani dhidi ya Raja Casbalanca tukafungwa mabao 3-0.”

“Safari hii niwaambie tu Vipers wamejichanganya kwani tutawapelekea pumzi ya moto na hakika lazima tupate matokeo mazuri ya kuwafurahisha Wanasimba wote ambao wamekata tamaa.”

“Bado tuna michezo miwili ya nyumbani, lazima tuitumie vizuri nafasi hii kwani naamini Simba kufika robo fainali ni kawaida kwake, hivyo Wanasimba tunawaomba mje kwa wingi kushangilia chama lenu ili tuwapige vizuri Vipers kwa Mkapa,” amesema Ahmed Ally

MCHAMBUZI: UTEUZI WA MO DEWJI NDANI YA SIMBA NI BATILI…KATIBA HAITAMBUI ALICHOFANYA… PAMOJA NA TFF KUTOA MAAMUZI….YANGA WAMLIMA BARUA NZITO FEI TOTO…MSIMAMO WAO HUU HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply