Habari za Yanga SC
Habari za michezo

KUELEKEA MECHI NA WAARABU…NABI ATAMBA YANGA KUUTIKISA M’BUYU…

admin March 13, 2023 7:26 pm

Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hawatarudia makosa kwenye mechi yao dhidi ya US Monastir kwa wachezaji wa timu hiyo kusaka matokeo mapema jambo linaoongeza nguvu ya kujiamini na kucheza kwa utulivu.

Timu hiyo inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa hatua ya makundi inasaka pointi tatu ili kufikisha malengo ya kutinga hatua ya robo fainali, ina pointi saba kwenye kundi D baada ya kucheza mechi nne.

Kituo chake kinachofuata ni dhidi ya US Monastri mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 19 wakiwa wanakumbuka kuwa walipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0.

Nabi alisema kuwa kuna ugumu kwenye mashindano ya kimataifa kutokana na kila timu kuhitaji ushindi hivyo watajitahidi kupata matokeo mapema kuongeza nguvu ya kujiamini.

“Ikiwa tunakutana na timu imara ambayo inahitaji matokeo ni lazima tufanye kazi kubwa kwenye kutumia nafasi hasa zile za mwanzo zitatufanya tuwe imara na kupata matokeo mazuri.

“US Monastir ni timu imara ina wachezaji wazuri hata wachezaji wetu nao ni wazuri hivyo makosa ambayo tulifanya kwenye mchezo uliopita tunayafanyia kazi,” alisema Nabi.

WAKATI YANGA WAKIJITAFUTA …..SIMBA YAZIDI KUTAKATA CAF…WAIPITA TP MAZEMBE KWA KILA KITU… WAKATI HOROYA WAKIPANIA KUMALIZA KAZI DAR…MBRAZILI SIMBA KUINGIA NA SAPRAIZI HII …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply