YANGAKULITETEA TAJI LAO...TUMEWAACHA POINTI NYINGI WANAOTUFATA...TUNAPAMBANIA MATAJI YOTE
Ligi Kuu

YANGA KULITETEA TAJI LAO…TUMEWAACHA POINTI NYINGI WANAOTUFATA…TUNAPAMBANIA MATAJI YOTE

Marce Ben Komba March 15, 2023 12:24 am

Pointi 8 ambazo wamewaacha watani zao wa jadi Simba, zimeipa kiburi Yanga ya kufanya vizuri kwenye mechi zijazo za Ligi Kuu Bara na kutetea taji lao.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 65, huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi 57, zote zikiwa zimecheza mechi 24.

Akizungumza na SOKA LA BONGO, Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga, alisema: “Ni pointi nyingi ambazo tumewaacha wale wanaotufuata, bado tuna mechi mbele yetu, tutapambana kushinda zote ili kutetea taji letu.

“Kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya kupambania mataji ambayo tunatetea ikiwa ni pamoja na ligi, hili ni muhimu kwetu ukizingatia tunaongoza katika msimamo, tunaamini kwamba tutafikia malengo yetu.”

SABABU ZA FEISAL SALUM “FEI TOTO” KUITWA STARS…”YUPO FIT SANA LICHA YA MATATIZO…MCHEZAJI MZURI ATATUSAIDIA KMC YATANGAZA VITA…MASHABIKI MGUU PANDE MGUU SAWA…TUNAZIDI KUWA IMARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply