Feisal Salum FEI TOTO
Habari za michezo

MANARA AMTAFUTIA TIMU ULAYA FEISAL SALUM “FEI TOTO”…KULIPWA MIL 300…

Marce Ben Komba March 28, 2023 8:56 am

Sakata la kiungo wa Yanga Feisal salum ‘Fei Toto’ limezidi kushangaza wengi baada ya kuibuka kwa mzee Sunday Manara ambaye amefunguka kila kitu kuhusu mchezaji huyo.

Feisal ambaye alifanya jaribio la kufunja mkataba wake mnamo mwezi Desemba 2022, na jaribio hilo lilikwama baada ya viongozi wa Yanga kuweka ngumu kwa kumrudishia Feisal milioni 112 ambazo alizipeleka ili kuvunja mkataba huo.

Yanga ilipeleka shauri hilo katika kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya TFF na hukumu ilitoka ikibainisha kuwa Feisal ni mchezaji halali wa Yanga.

Mzee Sunday Manara amefunguka na kueleza kuwa Feisal alishawishiwa kwa kiasi cha fedha ili kuondoka Yanga lakini pia mama wa mchezaji huyo naye aliingia mkenge

“Fei Toto sasa hivi ana miaka 27, Fei Toto hivi alivyo anaweza kucheza klabu yoyote ya Ulaya, kwa udhaifu wa kuwa maskini ya Mungu hana upeo mkubwa na mama yake hana upeo mkubwa, wamemshawishi kuwa utapata hela milioni mbili tatu ondoka Yanga bila hata kufuata sheria na wakamdanganya, bwana wewe hela wanazodai hizi hapa warudishie.

“Mimi niliwahi kumpigia simu Fei Toto na kumuomba nimsaidie kumsapoti na kuna watu kutoka Ulaya wameniambia wapo tayari kumlipia Fei Toto milioni 300 kama atakubali, kwa Sababu wanaamini kabisa ana uwezo lakini hana ushauri na bahati mbaya hawa watu hawamtakii mema.

“Mtu angezingatia ana miaka 27 akitoka hapa acheze mpira labda acheze Simba, lakini labda akienda Azam inacheza na timu kubwa labda na Mtibwa labda na Prisons au Geita Gold wale, sio lengo la Fei Toto kwa uwezo ule, uwezo wa Fei Toto ni viwanja kama vya Mali vya Morocco vinazidi kumtia katika soko la mpira Ulaya,” alisema mzee Manara.

MAGAZETI: SIMBA YAVAMIA KAMBI YA TAIFA STARS…MORRISON AMEZUA JIPYA YANGA HILI HAPA KIUNGO MNIGERIA AWAGOMEA SIMBA…MABOSI WACHANGANYIKIWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply