Habari za Simba SC
Habari za michezo

HIZI HAPA SALAMU ZA SIMBA KWA YANGA….ZATINGA AVIC TOWN KIBABE….

admin April 11, 2023 3:59 pm

Hii ni kusema kuwa Simba wameamua kuwatumia salamu za wazi watani zao Yanga na wapinzani wao wengine kwa kimataifa, wakidai mchezo wao na Raja Casablanca wamepata somo la kuwamaliza wapinzani.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa, mchezo wao na Raja ulikuwa ni kipimo tosha cha kuona ni kiasi gani watakwenda kuwavuruga wapinzani kwenye mechi zao ngumu zijazo.

Ally alisema, walichojifunza Morocco ni mbinu za ndani na nje ya uwanja, kwa maana benchi la ufundi limepata mbinu mpya na kwa upande wa mashabiki wamepata somo ambalo linakuja kutumika kwenye mechi zao ili kuwavuruga wapinzani.

โ€œTulifungwa mabao 3-1 na Raja Casablanca, tunajivunia sana mchezo ule kwa sababu umetufunza mambo mengi na kutupa picha ya kuiendea michezo yetu migumu.

โ€œBenchi la ufundi limeondoka na kitu, mimi nimepata jambo ambalo nakwenda kufanya na mashabiki wangu kwenye kushangilia ili kuwavuruga wapinzi.

โ€œWote waliona namna ambavyo mashabiki wa Raja walivyokuwa wanachizika. Ile sasa nataka ije Simba, nataka wapinzani wavurugwe,โ€ alisema Ally.

Aprili 7, mwaka huu, Simba watacheza na Ihefu kwenye mchezo wa robo fainali ya Azam Sports Federation Cup, kisha Aprili 10 dhidi ya timu hiyo ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara. Baada ya hapo, ni dhidi ya Yanga katika Ligi Kuu Bara, Aprili 16.

KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA YANGA…HAWA HAPA MAREFA WA MCHEZO HUO KELVIN YONDANI AMPIGIA SALUTI MSHAMBULIAJI YANGA…AMEZUNGUMZA HAYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply