Habari za Yanga SC
Habari za michezo

MASTAA YANGA SC WATUA KISHUA NIGERIA….RIVER UNITED WAPAGAWA…

admin April 21, 2023 6:23 pm

Msafara wa watu 49 wa kikosi cha Yanga SC, umetua salama jioni ya leo kwenye mji wa Lagos, Nigeria.

Yanga SC imesafari Nigeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF, dhidi ya wenyeji wao Rivers United.

Msafara huo uliondoka Dar Es Salaam, kwenye uwanja wa ndege wa Julias Kambarage Nyerere alfajiri ya leo kwa ndege ya shirika la Ethiopia.

Hapa Lagos, Yanga itaweka kambi ya siku moja kabla ya kesho asubuhi kuondoka kuelekea mji wa Uyo, utakapopigwa mchezo huo siku ya Jumapili, saa 10:00 kwa saa za Tanzania.

Tukiwa hapa Lagos, kikosi kitafanya mazoezi ya kuweka mwili sawa usiku leo kisha kupumzika kujiandaa na safari ya kesho.

Akizungumza na YANGA MEDIA, meneja wa kikosi cha Yanga, Waleter Harrison amesema, “Safari imekuwa nzuri hatujapata changamoto kubwa njiani. Kila kitu kimekwenda sawa kabisa.

“Tutakuwa na ratiba ya mazoezi leo usiku kisha wachezaji watampuzika kujiandaa na safari siku ya kesho asubuhi,” alisema Walter.

MUZIKI WA YANGA WAITISHA RIVERS UNITED…KIUNGO SIMBA AMPGIA SIMU MAYELE MASTAA SIMBA MGUU PANDE MGUU SAWA…WYDAD TUMBO JOTO…KOCHA AFUNGUKA HAYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply