BONDIA ALIYEANGUKA ULINGONI...AFARIKI DUNIA AKIPATIWA MATIBABU
Burudani

TANZIA:BONDIA ALIYEANGUKA ULINGONI…AFARIKI DUNIA AKIPATIWA MATIBABU

Marce Ben Komba April 28, 2023 7:57 am

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Najum kutoka jijini Mbeya amefariki Dunia mchana wa leo katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma (General) alipokuwa akipatiwa matibabu.

Najum alianguka ulingoni Jumapili iliyopita baada tu ya kumalizika kwa Pambano lake la raundi nne dhidi ya bondia wa Dodoma Laurent Segu, na kuwahishwa hospitali ambapo inaarifiwa alifanyiwa upasuaji mdogo wa kichwa hadi Asubuhi ya leo hali yake ilizidi kuimarika kabla ya kufikwa na mauti mchana wa leo.

Bondia huyo alikuwa amecheza mapambano matatu tu ya ngumi za kulipwa pamoja na hilo la Jumapili iliyopita, ambapo ameshinda Moja na kupoteza mawili.

Mwamuzi na Jaji wa kimataifa wa Tanzania, Pendo Njau ambaye alikuwa karibu na Bondia huyo amesema: “Ni kweli Ibrahim amefariki mchana wa leo saa sita alipokuwa amelazwa, nimepokea taarifa kutoka kwa Mama Sophia Mwakagenda ambaye ndiyo alikuwa promota.

“Sasa mwili ushatolewa hospitali wanaelekea Kyela Mbeya kwa ajili ya mazishi,”

MO AINGILIA KATI SHOO YA WAARABU…NABI AWAANDALIA SAPRAIZ HII RIVERS,…. HUYU HAPA REFA ATAKAYECHEZESHA MECHI YA YANGA…KUMBE ALICHEZESHA MECHI YA PSG NA INTER

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply