Habari za Yanga SC
Habari za michezo

KUHUSU KUIKOSESHA TIMU MAGOLI JUZI…NABI ASHINDWA KUJIZUIA KWA MZIZE…

admin May 2, 2023 2:59 pm

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Nasreddine Nabi amemtetea kinda wake, Wari Clement Mzize akisema kuwa alicheza vizuri kwenye mchezo wao dhidi ya Rivers United licha ya kukosa nafasi mbili za wazi juzi Aprili 30, 2023 katika DImba la Mkapa.

Nabi amesema hayo mara baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuiondoa Rivers United ya Nigeria huku baadhi ya wadau na mashabiki wa soka wakidai kuwa Mzize hakucheza vizuri kwani ameinyima timu yake ushindi kwa kukosa nafasi za wazi.

“Mimi kwa upande wangu sijaona kama amecheza vibaya, ni kijana wa Kitanzania ambaye tunamtengeneza, ikipatikana nafasi unampa ili uone atafanyaje.

“Alitengenezewa vizuri akapata nafasi mbili, moja ikapita juu na nyingine pembeni, alikuwa kwenye movement na amesaidia pia kukaba. Mimi naona amecheza vizuri kutokana na umri wake jinsi ulivyo,” amesema Nabi.

Wachezaji saba wa Tanzania walioanza kwenye kikosi cha Yanga SC  dhidi ya Rivers United ni;

1. Dickson Job
2. Kibwana Shomari
3. Ibrahim Baka
4. Bakari Mwamnyeto
5. Mudathiri Yahya
6. Salum Aboubakar
7. Clement Mzize.

Yanga SC itakutana na Marumo Gallants katika hatua ya nusu fainali ambapo mchezo wa kwanza utapigwa katika dimba la Mkapa, Mei 10, 2023 kisha mchezo wa marudiano utapigwa nchini Afrika Kusini Mei 17, mwaka huu.

PAMOJA NA SIMBA ‘KUBUTULIWA’ MOROCCO…MBRAZILI SIMBA APEWA ‘KONGOLE’…. ISHU YA BEKI MPYA YANGA KUTOONEKANA …UKWELI WAANIKWA WAZI….MWAMNYETO ATAJWA KUWA CHANZO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply