Habari za Yanga SC
Habari za michezo

KUHUSU SAKATA LA FEI TOTO….MWAMBUSI ‘AIFYTUKIA’ YANGA….AWAPA ‘MAKAVU LIVE’….

admin May 9, 2023 11:37 am

Aliekuwa Kocha wa Yanga Juma Mwambusi ameisihi Klabu hiyo kumuachia kwa moyo mkunjufu Kiungo wao Feisal Salum ambae yupo kwenye mgogoro na Klabu hiyo akitaka kuvunja Mkataba.

Akizungumza Mwambusi amewataka Yanga kumruhusu Feisal ili akacheze mpira hasa baada ya kukaa muda mrefu pasipo kuonekana Uwanjani.

“Yanga wamuachie tu kijana aondoke. Busara inabidi itumike maana yanga wanafanya vizuri hata bila ya Feisal wamuachie aondoke waokoe kipaji chake maana hata taifa linanufaika na kipaji chake”

“Busara itumike, sawa sheria zipo lakini manufaa ni kwa mtoto, maana anakaa bila kucheza anaharibu kipaji chake, viongozi wa Yanga wafikirie mara tatu, waweke jambo hili likae sawa maana taifa linamtegemea Feisal”

Feisal mara kadhaa amegonga mwamba katika harakati zake za kutaka kuvunja Mkataba na Yanga.

MAMBO YAZIDI KWENDA KOMBO KWA MWAKINYO…AZIDI KUPOROMOKA KWENYE VIWANGO VYA DUNIA… WAKATI AWESU WA KMC ‘AKIENJOY’ NA JAMII….NA WEWE VUTA MTONYO KUTOKA MERIDIANBET…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply