Habari za Simba SC
Habari za michezo

MABOSI SIMBA KUWAJADILIA MBRAZILI NA MGUNDA…LOLOTE LINAWEZA KUTOKEA….

admin May 11, 2023 10:59 am

Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, imepanga kukutana kwa ajili ya kulifanyia tathimini Benchi la ufundi la timu hiyo, linaloongozwa na Kocha Mkuu, Mbrazili, Roberto Oliveira β€˜Robertinho’.

Hiyo ni baada ya Simba kutoka kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Azam katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports uliopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema mara baada ya mchezo dhidi ya Azam FC, haraka uongozi utakutana kufanya tathimini ya kila kiongozi wa Benchi la Ufundi.

Ally alisema upo uwezekano mkubwa wa kuingiza maingizo mapya ya viongozi wa benchi la ufundi katika msimu ujao wenye maono na kuifikisha pazuri katika michuano ya kimataifa.

AHMED ALLY:- TULIPOFELI NA KUANGUKA NI PALE TULIPOSAJILI WATU TULIOWAAMINI… KUELEKEA USAJILI MPYA SIMBA….HAWA HAPA MASTAA 10 WANAOTAKIWA KUPIGWA CHINI HARAKA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply