Habari za Simba SC
Habari za michezo

KUHUSU KUTEMWA SIMBA…MGUNDA AVUNJA UKIMYA …AANIKA MSIMAMO WAKE…AITAJA COASTAL UNION..

admin June 17, 2023 11:43 am

Kocha kipenzi cha mashabiki wa Simba, Juma Mgunda amefafanua maneno yanayotembea mitandaoni kwamba si sehemu ya kikosi kipya cha Mnyama.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Mwanaspoti kujiridhisha kwamba Kocha Robertinho, amewaambia Simba wampe mkataba Mnyarwanda, Hategekimana Corneille wa Rayon kama Kocha wa viungo lakini awali akiwa nae Rwanda alikuwa akimtumia kama mshauri wake.

Mgunda ambaye ni mzoefu mwenye na miongoni mwa wazawa wasomi akiwa na leseni A ya CAF, amesema kuwa bado yupo sana Simba, akizikana tetesi za kutaka kurejea kwenye timu yake ya zamani Coastal Union ya Tanga.

Amefafanua kwamba kwanza Coastal licha ya kuwa washikaji zake lakini ana matatizo nayo binafsi ambayo hakutaka kuyaweka wazi.

Mgunda ambaye kwa sasa yupo mapumzikoni Tanga baada ya kumalizika msimu wa Ligi Kuu Bara amesema bado ataendelea kuwatumikia wana Msimbazi hadi mkataba wake utakapomalizika ndipo atakapojua kinachofuata na bosi wake, Robertinho hajamwambia kama kuna mabadiliko yoyote kwenye kibarua chake.

“Mmefanya vizuri kuniuliza, kwani majibu yangu yatawapa kujua bado ni mfanyakazi wa Simba. Kuhusu Coastal siwezi kukataa kwamba ni timu yangu ambayo nimetoka nayo mbali, tukirekebisha matatizo yetu tutaendelea salama,” alisema kocha huyo ambaye amejiwekea rekodi nzuri Simba.

“Nipo Tanga kwa mapumziko utakapofika muda wa kurejea kwenye majukumu Simba mashabiki wangu wataniona,”alisema na kuongeza kuwa msimu uliomalizika aliuona ushindani mkubwa ambao unawapa picha ya kufanya maandalizi makubwa zaidi kwa ajili ya ujao.

“Ligi ina ushindani mkali na soka linakuwa, hivyo kila timu itakuwa inajipanga kulingana na mahitaji yake ya msimu mwingine,”alisema.

Mgunda ana mchango mkubwa Simba, aliivusha kipindi anakaimu ukocha mkuu baada ya kuondoka Zoran Maki, aliitengeza timu licha ya kushinda mechi nyingi za Ligi Kuu pia alifanya vizuri kimataifa.

HAKUPOTEZA CAF

Big Bullets 0-2 Simba (Sept 10/2022)

Simba 2-0 Big Bullets (Sept 14/2022)

Primeiro de Agosto 1-3 Simba (Oktoba 9/2022)

Simba 1-0 Primeiro de Agosto (Oktoba 16/2022)

ASFC

Simba 8-0 Eagle

Simba 1-0 Caostal

RATIBA YA NGAO YA JAMII MSIMU UJAO HII HAPA….SIMBA WAPEWA MFUPA MGUMU…YANGA MHH.. HUYU NDIO MORRISON….’CHIZI’ MWENYE KIPAJI CHA MPIRA…MATUKIO YAKE TATA HAYA HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply