Habari za Yanga leo
Habari za Yanga

HIVI NDIVYO YANGA NA RAIS SAMIA WALIVYOAMSHWA SHANGWE LA ‘KUFA MTU’ JANA MALAWI…

Staff Desk July 6, 2023 10:26 am

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Malawi Dk Lazarus McCarthy Chakwera, wamekutana na kikosi cha Yanga kilichowasili Julai 5, 2023 nchini Malawi kwa mualiko maalumu wa Rais wa nchi hiyo.

Rais Samia amekutana na timu hiyo wakati akiwasili nchini Malawi ambapo amehudhuria sherehe za miaka 59 ya uhuru wa taifa hilo zitakazofanyika Julai 6, 2023.

Kikosi cha Yanga kimeshiriki katika mapokezi ya Rais Samia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu Lilongwe nchini Malawi.

Yanga wapo nchini humo ambapo watashiriki sherehe za miaka 59 ya Uhuru wa taifa hilo kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Nyasa Big Bullets ya nchini humo.

ISHU YA MAYELE KUONDOKA AU KUBAKIA YANGA IKO HIVI…AGOMEA MSHAHARA WA MIL 34 KWA MWEZI.. ACHANA NA MASTAA WAPYA….MAKOCHA WAPYA WATAKAO MSAIDIA MBRAZILI SIMBA HAWA HAPA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply