Habari za Simba leo
Habari za michezo

BAADA YA YANGA KUZINDUA UZI WAO JANA…HII HAPA TAARIFA MPYA KUHUSU JEZI ZA SIMBA…

admin July 6, 2023 4:01 am

Kampuni ya Sunderland imesema itazindua kwa pamoja jezi zote za Klabu ya Simba za mashindano ambayo wanashiriki kwa msimu wa 2023/24.

Jezi hizo ni za CAF Super League, Ligi ya Mabingwa Afrika, Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’, Ligi Kuu ya Wanawake na Ligi ya Vijana.

Akizungumza na Azam TV, mzabuni aliyeshinda zabuni ya kutengeneza jezi za Simba SC, Sunday Omar amesema tayari jezi hizo zipo nchini na klabu ndio watasema wanazindua lini.

Amemuomba Waziri wa Biashara na Viwanda, Mkurugenzi wa FCC, Polisi na mamlaka nyingine kusaidia kudhibiti jezi ‘Fake’ ili timu zinufaike na mapato yanayotokana na mauzo ya jezi zao.

Sunderland iliingia mkataba Sh bilioni 4 na Simba SC baada wa miaka miwili wenye thamani ya klabu hiyo kumalizana na Kampuni ya Vunja Bei iliyoingia nao miaka miwili iliyopita ukiwa na thamani ya Sh bilioni 2.

SINGIDA FG WAAMKA….WAANZA KUZIBOMOA SIMBA NA YANGA…KUANZA NA MASTAA HAWA… ROBERTINHO AYAPA MAJEMBE MAPYA SIMBA MASAA 270…JEMBE JIPYA YANGA LAANZA KAZI KIBABE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply