Habari za Yanga
Habari za michezo

WAKATI SIMBA NA AZAM WAKIWA NNJE…. YANGA ‘WAFUKUZWA’ AVIT TOWN…ISHU IKO HIVI…

admin July 20, 2023 3:42 pm

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Saleh Ally ‘Jembe’ amesema kuwa Yanga walitakiwa kutoka na kwenda kuweka kambi nje ya Tanzania badala ya kuendelea kusalia nchini kwa miaka mitatu mfululizo.

Jembe ametoa kauli hiyo akisema pia kuwa kutoka kwao nje kungewasaidia kubadilisha mazingira na kuwaweka sawa kisaikolojia.

“Yanga wangeondoka Avic Town wakaenda kutafuta mazingira mengine lakini yawezekana wao wameona faida ya pale.

“Misimu miwili wamebaki Avic Town na wamefanikiwa kuchukua kila kitu japo walizidiwa vitu vichache kama idadi ya mabao ya kufungwa, mechi za kufungwa na mabao ya kufunga.

“Nashauri Yanga watoke kwa sababu wamekaa pale muda mwingi sana, hata Ulaya mfano Real Madrid wana kila kitu lakini wanalazimika kutoka nje ya Hispania na kwenda Marekani kuliko kuwa pale pale wachezaji wanalala vyumba vilevile.

“Kwa upande wa Simba watakuwa na deni kwa sababu walipewa kambi nje ya Tanzania na timu ikashika nafasi ya pili, hawakuondoka na kombe lolote,” amesema Jembe.

BARBARA AZIDI KUKINUKISHA HUKO….ATUPA DONGO JIPYA KWA MO DEWJI…. BAADA YA YANGA KUMCHUKUA MKUDE, SIMBA YAMLETA MBADALA WAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply