Habari za Michezo
Habari za michezo

BAADA YA KUTOKA YANGA, HUYO MEYELE KAMA MFALME MCHEKI HAPA

Staff Desk July 31, 2023 10:54 am

Mshambuliaji Fiston ametangazwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Pyramid FC inayoshiriki Ligi Kuu Misri kutoka klabu ya Yanga ya Tanzania.

Mayele anaondoka Young Africans SC baada ya kuwatumikia Wananchi kwa misimu miwili huku akimaliza nafasi ya pili kwenye kinyang’anyiro cha ufungaji bora kwenye msimu wake wa kwanza, 2021/2022 kabla ya kushinda kiatu cha mfungaji bora (magoli 17) kwenye msimu wake wa pili wa 2022/2023 sambamba na kuibuka mchezaji bora wa msimu (MVP) wa Ligi Kuu Tanzania.

Mayele anaondoka Yanga baada ya kuisaidia kutwaa taji la Ligi Kuu mara 2, FA Cup 2 Ngao ya Jamii mara mbili na kuisaidia Yanga kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia yao msimu 2022/2023 akiwa Mfungaji bora wa Michuano hiyo akimaliza na magoli 7.

GAMONDI AFANYA MAAMUZI MAGUMU KWENYE KIKOSI CHA YANGA, MAYELE ATAJWA USHINDANI WA MASTAA HAPO SIMBA SIO POA, MATOLA AMUIBIA SIRI MIQUISSONE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “BAADA YA KUTOKA YANGA, HUYO MEYELE KAMA MFALME MCHEKI HAPA”

  1. Daniel wilhard says:

    Uwe na Maisha mema mwamba huko ughaibuni,,

Leave a Reply