Habari za Yanga SC
Azam FC

AZIZ KI AFICHUA SIRI HII YA KUIFUNGA AZAM

Staff Desk August 11, 2023 1:50 pm

Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burkina Faso Stephen Aziz Ki, ametoboa siri kwa kusema Kocha Mkuu wa Young Africans Miguel Angel Gamondi alimpa maelekezo maalum kabla hajaingia uwanjani kuikabili Azam FC.

Young Africans juzi Jumatano (Agosti 09) iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii uliofanyika Uwanja wa CCM Mkwakwani, jijini Tanga.

Aziz Ki amesema Kocha Gamondi alimpa maelekezo ambayo aliyafanyia kazi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha anaisaidia timu kupata ushindi.

Amesema mchezo huo haukuwa rahisi na iliwachukua Young Africans hadi katika dakika za mwisho kupata matokeo, kitu ambacho walifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

“Nilipewa maelekezo maalumu na Kocha Gamondi, kwani kabla ya kuingia nilizungumza naye kwa muda.

“Tulilazimika kubadilisha mchezo na kuhakikisha tunapata ushindi, mchezo haukuwa rahisi kwa pande zote, kwani kila timu imefanya usajili wa kuhakikisha msimu mpya unakuwa tishio” amesema

Young Africans itacheza Fainali Jumapili (Agosti 13) dhidi ya Simba SC iliyotoa Singida Fountain Gate kwa changamoto ya mikwaju ya Penati 4-2 jana Alhamis (Agosti 10) katika Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga.

YANGA SASA AKILI YOTE KWASIMBA, MAANDALIZI YAKE SIO POA GAMONDI AWAPOTEZEA SIMBA, ASEMA HAYA KUHUSU YANGA KUKUTANA NA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply