Habari za Simba na Yanga
Habari za michezo

DOUMBIA NA YANGA MPAKA KIELEWEKE ISHU IKO HIVI

Staff Desk August 20, 2023 6:39 pm

Wakati wadau na mashabiki wa soka wakijiuliza hatima ya beki Mamadou Doumbia ndani ya Yanga kutokana na kutoonekana kikosini pia akiwa hajapewa ‘Thank You’ kama ilivyotokea kwa wengine, Mwanaspoti limepata taarifa za kuaminika kuwa hawajamalizana.

Yanga ilimsaini Doumbia katika dirisha dogo la msimu uliopita sambamba na kiungo Mudathir Yahya na mshambuliaji Kennedy Musonda ambao wanaendelea kukiwasha, lakini beki huyo raia wa Mali haonekani kikosini.

Baada ya Yanga kufanya siri na baadhi ya viongozi kuulizwa na kushindwa kuweka wazi juu ya Doumbia aliyesaini mkataba wa miaka miwili, mmoja ya vigogo wa timu hiyo (jina tunalo), amefunguka kuwa bado hawajamalizana, lakini wapo kwenye hatua nzuri na siku sio nyingi wataafikiana.

Chanzo hicho kilisema hatua iliyopo ni kumtafutia timu ili kumuuza ama kumtoa kwa mkopo na wako mbioni kukamilisha hilo.

“Bado tunatafuta njia nzuri ya kulimaliza hili. Kila upande umeafiki tulichokiamua na sasa kwa kushirikiana na uongozi wa mchezaji, tupo kwenye hatua za mwisho za kumpatia timu atakayocheza msimu ujao na hapo kuna mawili, kumuuza au kumtoa kwa mkopo,” kilisema chanzo hicho.

Kilichotokea kwa Doumbia ni kama kilichotokea kwa Gael Bigirimana aliyesajiliwa na Yanga msimu uliopita, lakini akatemwa dirisha dogo na kushindwa kuafikiana kiasi cha hivi karibuni kurejea kikosini kimyakimya au ilivyo kwa Peter Banda wa Simba inayeelezwa amempisha kipa Ayoub Lakred, huku akiwa bado yupo kikosini akisikilizia hatima ya kutafutiwa timu iwe kwa mkopo au kuuzwa.

ITUMIE SLOT YA FOXPOT KUKUSANYA MTONYO KWA KILA DAU UNALOWEKA KWENYE MKEKA WAKO.. KWA SIMBA HII, TATIZO NI MZAMIRU, ISHU IKO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply