Habari za Yanga SC
Habari za michezo

GAMONDI AFUNGUKA ISHU YA KONKONI KUANZIA BENCHI

Staff Desk August 26, 2023 12:20 pm

Kocha mkuu wa Klabu ya Young Africans, Miguel Gamondi ametaja sababu za kutomwanzisha kwenye mechi zake mshambuliaji wake mpya Hafiz Konkoni akisema kuwa bado anampika zaidi.

Gamondi amesema kuwa Konkoni ni mshambuliaji tegemeo hivyo lazima amlinde kwa kumuandaa vizuri kisaikolojia, kumuondolea presha kwa kumpa dakika chache kisha baadae akiiva ataanza kumtumia kama atakavyo.

“Ninampa muda mchache Mshambuliaji Hafiz Konkoni kwa sababu ya kumlinda.Mchezaji tegemeo anapaswa kuanza taratibu kama ilivyokuwa kwa Aziz Ki pamoja na Pacome Zouzoua ili kumtolea pressure ya mashabiki na wachambuzi mpaka atakapokuwa fit zaidi.

“Mashabiki na wachambuzi wanaweza ondoa ufanisi wa mchezaji. Taratibu ataingia kikosini na ataanza kucheza kwa dakika nyingi hivi karibuni,” amesema Kocha Miguel Gamondi.

Itakumbukwa kuwa Konkoni ambaye amesajiliwa kutoka Ghana alicheza mchezo wa (1) wa mashindano kwa dakika 8, akaja kucheza mchezo wa pili dakika 10 na dhidi ya KMC alicheza dakika 28 na kufunga bao moja na assist moja.

SKUDU ATOA KAULI NZITO BAADA YA KUREJEA NCHINI KWA PIRA HILI LA GAMONDI HATARI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply