Habari za michezo
INONGA ALISTAHILI JAMBO HILI
Staff Desk
August 27, 2023
3:37 pm
Henock Inonga Baka anaweza kuwa mchezaji ambae alihitaji zaidi mafanikio ya pamoja pale Simba hasa kwa namna ambavyo amekuwa akisifika kwenye nafasi yake dhidi ya walinzi wengine nchini.
Kwa bahati mbaya baadhi ya watu wamekuwa wakisubiri kuuimba zaidi ubora wa mtu mpaka pale unapokuwa umeambatana na mataji japo Inonga anastahili sifa zake bila hata hayo mataji.
Last season ukuta uliokuwa nae ndio uliruhusu mabao machache zaidi kwenye ligi na ameingia kwenye kikosi bora mara zote 2 alizoshiriki.
Ngao ya jamii aliyofanikiwa kushinda mwanzo wa msimu huu ni icing tu juu ya keki yake.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.