Habari za Yanga
Habari za michezo

MCHAMBUZI: YANGA WAHAJAFANIKIWA KIMATAIFA….LABDA SIMBA KWA KUWA WANA NGAO …

admin September 20, 2023 4:51 pm

Mchambuzi wa soka nchini, Farhan Kihamu amesema Yanga SC kufika fainali ya Shirikisho Afrika si mafanikio.

Amesema hata Simba SC nao hawajafanikiwa kwenye soko la Kimataifa bali wamepiga hatua.

“Yanga kufika fainali (CAFCC 2022/23) ni kupiga hatua hawajafanikiwa, timu zetu kwenye mashindano ya kimataifa hakuna aliyefanikiwa wamepiga hatua tu.

“Simba leo hii kuingia makundi sio stori, kucheza robo sio stori wenyewe wanahitaji nusu fainali, kuna siku watahitaji fainali na wakibeba ubingwa watakuwa wamefanikiwa,” alisema Farhan.

Aidha katika hatua nyingine, Farhan amesema mafanikio siko zote yanapimwa kwa mataji na sio kupiga hatua fulani katika mashindano.

“Klabu zetu zimepiga hatua hazijafanikiwa, kufanikiwa ni reward mfano Simba na Yanga msimu huu Simba ndio imefanikiwa (wamebeba ngao) mafanikio kwenye mpira ni kufika mwisho na kubeba taji.

“Timu zetu zinajitahidi zimepiga hatua, zamani timu ikienda nje inapigwa tatu nne zikirudi maelezo mengi lakini sasa hivi wiki mbili kabla wanajua watalala wapi watatumia usafiri gani hizi ni hatua sio mafanikio,” alisema Farhan.

NAMNA MTZ NOVATUS MIROSHI ALIVYOKICHAFUA JANA LIGI YA MABINGWA ULAYA… JINA LA CHAMA LANUKIA CAF….ISHU NZIMA INATEGEMEANA NA MAISHA YAKE NA SIMBA,…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply