Habari za michezo

KIUNGO WA YANGA MAMBO MAGUMU

Staff Desk September 23, 2023 6:52 pm

 

Kiungo wa zamani wa Yanga, Abdulaziz Makame ‘Bui’, baada ya kukosa timu ya kuichezea anapigia mahesabu usajili wa dirisha dogo, huku akieleza anavyotakiwa kujitoa kuhakikisha analinda kiwango chake.

Makame aliyewahi kuichezea Yanga, Namungo na Kagera Sugar alisema kuna wakati anatafuta makocha wanaomsaidia kumnoa kiwango chake, wakati mwingine anajichanganya na mechi za mtaani, ili mradi kiwango chake kisishuke, ili akirejea kazini asianze upya.

“Siwezi kusema kwasababu nipo nje ya majukumu basi najiachia, najitambua na najua nataka nini kwenye soka, ingawa si rahisi inahitaji kujitoa kwani hakuna mtu anayekulazimisha kufanya mazoezi tofauti na inavyokuwa kwenye timu,” alisema na kuongeza; “Zipo sababu nyingi za kukosa timu, wakati mwingine yanakuwa maslahi, ingawa siwezi kueleza kila kitu, kikubwa najipanga kwa ajili ya wakati mwingine, kazi yangu ni soka na bado nina umri wa kucheza mpira na kila hatua wangu ni funzo,” alisema Bui.

FEI TOTO AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA HALI YAKE AZAM MAXI, PACOME WATISHA WASUDANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply