Tanzania imeweka historia kwa mara ya kwanza timu zake mbili kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hii ni baada ya mapacha wa Kariakoo, Simba SC na yanga Sc kufanikiwa kutinga hatua hiyo kwa pamoja ndani ya msimu mmoja.
Yanga wametinga hatua hiyo maada ya kushinda hatua ya kwanza ya awali kwa kuifunga ASAS FC ya Djibouti kwa mabao 2-0 ugenini na 5-1 nyumbani (jumla ya bao 7-1), kisha hatua ya pili ya awali kuwafunga Al-Merrikh ya Sudan mabao 2-0 ugenini na bao 1-0 nyumbani (jumla ya bao 3-0).
Kwa upande wa Simba SC wao hawakuanzia hatua ya mwanzo, badala yake walianzia hatua ya pili ya mtoano na kutoa sare ya bao 2-2 ugenini dhidi ya Power Dynamos na jana wakatoa sare ya bao 1-1 wakiwa nyumbani (jumla ya sare 3-3) hivyo wamefanikiwa kuingia makundi kwa kanuni ya bao la ugenini.
Msimu uliopita, Simba ilikuwa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ilitolewa katika hatua ya robo fainali baada kwa mikwaju ya peanti dhidi ya Raja Casablanca.
Yanga wao msimu uliopita walicheza mpaka fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kuibuka washindi wa pili kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya kutoa sare ya bao 2-2 na USM ALger ya Algeria.
Simba na Yanga wanaweza kukutana kwenye hatua ya Makundi ya michuano hiyo kwani Simba wapo Pot namba 2 wakati Yanga wakiwa pot namba ipo Pot 3, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa miamba hao wa soka nchini Tanzania kukutana kwenye kundi moja.
Draw ya CAF CL & CC Itafanyika Ijumaa, October 6 Johannesburg Africa Kusini, Kila timu imepangwa kwenye POT yake kutokana na wingi wa alama zake kwa kipindi Cha miaka mitano [5] iliyopita.
Simba POT 2 [35]
Yanga POT 3 [20]
Timu 15 mpaka sasa zimeshafuzu hatua ya Makundi ya CAFCl na bado timu moja tu inayosubiriwa baada ya mchezo wa leo kati ya CR Belouizdad na Bo Rangers ambapo matokeo ya mchezo wa awali Bo Rangers ilifungwa bao 3-1.
Al Ahly
Pyramids
Jwaneng Galaxy
TP Mazembe
Petro Luanda
ES Tunis
Medeama
Mamelodi
Yanga SC
Etoile Sahel
Wydad AC
Simba SC
ASEC Mimosas
Al Hilal
Nouadhibou
Belouizdad or Bo Rangers
Kundi atakalokuwepo Simba na atakalokuwepo Yanga litakua na mpinzani mmoja kutoka hapa.