Habari za Yanga
Habari za michezo

HERSI ATOBOA SIRI YAYANGA NA MAKAMPUNI HAYA

Staff Desk October 5, 2023 6:43 pm

Rais wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Hersi Said amesema kufanya vizuri kwa klabu hiyo kuanzia uwanjani hadi kwenye utendaji wao, kumezivutia kampuni kubwa kujitokeza kufanya nao kazi.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Hersi amesema licha ya kuridhika na wadhamini walionao, kuna wengine wawili wamejitokeza kuwekeza fedha zao na hivi karibuni watawekwa hadharani.

“Tunakwenda kusaini mkataba na makampuni makubwa mawili katika kipindi cha majuma mawili yajayo, yamevutiwa na utendaji kazi wetu na mafanikio yetu ya uwanjani na yanatamani kufanya kazi na sisi,” amesema

Kutokana na hilo, Hersi ameipongeza idara ya masoko, habari na vitengo vyote vya klabu hiyo akisema kila mmoja amefanya jukumu lake vizuri hadi kuwa kwenye mafanikio makubwa kipindi hiki.

Amesema kwa sasa kuna utofauti mkubwa wa mafanikio ukilinganisha na miaka miwili iliyopita na hiyo yote ni kutokana na maboresho ambayo wamekuwa wakiyafanya kuanzia kwenye benchi la ufundi, wachezaji na idara zote.

FT: TZ PRISONS I-3 SIMBA SC…..BOCCO KAMA KAWA….MBRAZILI ACHEKELEA ‘KOONI’… ANGUKO LA YANGA DHIDI YA IHEFU WA KULAUMIWA HUYU HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply