Habari za Simba
Habari za michezo

KWA UPANDE HUU SIMBA PASUA KICHWA

Staff Desk October 26, 2023 5:53 pm

Katika mechi tano mfululizo walizocheza Simba hawajaambulia clean sheet, (kucheza bila kuruhusu bao) zaidi ya kutunguliwa mabao sita.

Makosa yapo katika eneo la kiungo anapocheza Mzamiru Yassin, Fabricne Ngoma, beki anapocheza Henock Inonga, Che Malone, mlinda mlango Ally Salim, Ayoub Lakred.

Ni Ally Salim kosa lake kubwa ni katika kupangua mipira langoni mwake mingi inaishia katika eneo alilopo inakutana na wapinzani.

Ilikuwa hivyo dhidi ya Al Ahly, Uwanja wa Mkapa. Ongeza kosa lingine Timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira katika hatua ya robo fainali ya African Football League iliruhusu mabao matatu dhidi ya Al Ahly.

Mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 2-2 Al Ahly na ule wa pili ilikuwa Al Ahly 1-1 Simba na wakaondolewa kwa kanuni ya mabao ya ugenini ikiwa ni faida kwa Al Ahly.

KIKOSI CHA YANGA KIPO TAYARI KWA AJILI YA SINGIDA GAMONDI ATIA NENO HILI BAADA YA UKIMYA MREFU….GOMES HUYU HAPA…SHAVU LAKE JIPYA NI ZAIDI YA SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply