Habari za michezo
YANGA WAMCHUNGE SANA HUYU MWAMBA LIGI YA MABINGWA
Staff Desk
November 12, 2023
10:33 am
Mtangane kati ya CR Belouizdad wapinzani wa Yanga kwenye CAFCL kwa dakika 90 dhidi ya USM Alger umemaliziks na CR wamefungwa bao 2-1 wakiwa ugenini.
Kiufundi CR Belouizdad inaonekana ni timu ambayo inacheza kwa kasi kubwa wakishambulia kutokea pembeni wakitegemea uwezo mkubwa wa mawinga wao kupiga krosi.
Katika krosi ambazo wanapiga wanategemea uwezo mkubwa wa mshambuliaji wao Leonel Wamba ambaye anauwezo mkubwa wa kufunga kwa vichwa.
Wamba raia wa Cameroon mwenye umri wa miaka 21,mpaka sasa kwenye mashindano yote amefunga mabao 5 huku 3 yakiwa ya kichwa.
Yao Yao na Lomalisa kule pembe, wamchunge sana huyu Wamba Novemba 24, vinginevyo atawatesa wananchi.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.