Habari za michezo

KIPIGO CHA 1-5 CHAMPONZA AMINA APOKEA KIFINYO

Staff Desk November 12, 2023 10:41 am

Amina Ndunguru (39) Mkazi wa Makoka, amenusurika kifo baada ya kujeruhiwa vibaya kichwani hususani sehemu ya jicho la kushoto, kutokana kipigo kinachodaiwa kufanywa na mume wake, Charles Kulemba.

Mama huyo wa watoto wanne maarufu kwa jina la Mama Vai, amelazwa katika Hospitali ya Bochi iliyopo Mbezi kwa Msuguri, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Amina alikutana na kipigo hicho mara baada ya kuonesha furaha ya ushindi wa mabao 5-1 ambao Yanga iliupata kwa kumwadhibu mtani wake wa jadi Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliofanyika Jumapili Novemba 5, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Amina ni shabiki wa Yanga na Mume wake ni shabiki wa Simba.

“Ndugu mwandishi, kilichoniponza mimi ni Yanga, tuliwapiga Makolo 5-1,” anasema Amina kwa shida akiwa Wodi ya Wanawake ghorofa ya pili, Jengo namba mbili hospitalini hapo.

YANGA WAMCHUNGE SANA HUYU MWAMBA LIGI YA MABINGWA UNAAMBIWA HUKO JANGWANI NI MWENDO WA SUPU TU ……. HERSI ATOA CHAPATI 5000

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply