Habari za michezo
Habari za michezo

KISASI CHA 5G KULIPWAAA!!?…..TFF WAZIKUTANISHA TENA SIMBA NA YANGA….

admin November 23, 2023 8:34 pm

Kikosi cha timu ya wanawake cha Yanga, Yanga Princess kinatarajiwa kucheza dhidi ya Simba Queens katika mchezo wa Ngao ya Jamii Wanawake hatua ya nusu fainali.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Yanga Princess itapambana na Simba Queens Desemba 9, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Mshindi wa mechi hiyo atacheza fainali dhidi ya mshindi wa nusu fainali nyingine kati ya JKT Queens na Fountain Gate Princess.

Mechi hizo za Ngao ya Jamii, ni ishara ya ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake 2023-2024.

Fainali ya Ngao ya Jamii Wanawake itachezwa Desemba 12, 2023, kabla ya mchezo huo wa fainali, mapema itapigwa ya kumsaka mshindi wa tatu. Mechi zote hizo zitachezwa Uwanja wa Azam Complex.

KUELEKEA MECHI NA ASEC ….MASTAA HAWA SIMBA WAPEWA ‘HIRIZI’ ZA MCHEZO MAPEMAAA…. NGOWI:- JEZI ZA YANGA KWA MISIMU MITANO IJAYO ZIKO TAYARI…..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply