Habari za Simba leo
Habari za michezo

MASHINE INGINE YA KAZI HII HAPA….SIMBA KUMLIPA MSHAHARA KUFRU…, BALEKE, PHIRI BYE BYE…

admin January 16, 2024 12:34 am

SIMBA imemtambulisha nyota mwingine wa kimataifa kutoka nchini Ivory Coast, Freddy Michael Kouablan akitokea klabu ya Green Eagles ya Zambia.

Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kutumika Simba katika kuimarisha safu ya ushambuliaji ambayo.Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdelhak Benchikha akihitaji kuongezewa mshambuliaji.

Katika mkatana huo, inaelezwa kuwa Freddy atakuwa analipwa mshahara wa Dola 6500 sawa na Milioni 16.25 kwa mwezi, huku akihakikishiwa usafiri na nyumba ya kuishi nnje ya kambi ya timu.

Kouablan hadi sasa ndiye anaongoza kwa ufungaji kwenye ligi kuu ya Zambia kwa kuweka kambani mabao 14 na assist 4 katika michezo 17 aliyocheza.

Usajili wa nyota huyo umekuja saa chache baada ya kutangaza mshambuliaji mwingine Pa Omar Jobe akitokea katika klabu ya FC Zhence inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kazakhstan.

Ujio wa nyota hao unazidi kuhatarisha nafasi za washambuliaji wawili wa Simba, Jean Baleke na Mosses Phiri kuendelea kutumikia kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Hata hivyo inafahamika kuwa Jean Baleke atajiunga na FC Goliath ya Bangladesh, huku Moses Phiri yeye ikiwa bado haijajulikana ataenda klabu gani japo vyanzo vyetu vya habari vinadai kuwa huenda akarudi kwao Zambia.

PHIRI, BALEKE ‘WAWEKEWA PANGA SHINGONI’…BENCHEKH AWAKATAA HADHARANI…MANGUNGO ATIA NENO.. YANGA WAIJIBU SIMBA KWA KISHINDO….WASHUSHA MASHINE HII YA KAZI KUTOKA ULAYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply