Habari za Yanga leo
Habari za michezo

MOLOKO BADO YUPO AISEEE…..ISHU YAKE MPYA HII HAPA….

admin January 16, 2024 9:03 pm

Saa chache baada ya Yanga kutangaza kumtema winga Jesus Moloko Geita Gold iko naye mezani kwa mazungumzo ya kumsajili kwa mwaka mmoja.

Geita inamtaka Moloko kwenda kuongeza nguvu kwenye kikosi chao ikiutazama uzoefu wake na nidhamu kubwa aliyoonyesha akiwa Yanga.

Geita inapambana na Rayon Sport ya Rwanda kuwania saini ya winga huyo wa zamani wa AS Vita na Union Maniema zote za DR Congo.

Moloko ametemwa na Yanga kupisha usajili wa winga Mghana Augustine Okrah aliyetua klabuni hapo akitokea Bechem United ya nchini kwao.

Kwasasa Geita inapambana na Moloko juu ya mshahara wake na maslahi mengine binafsi wakati mazungumzo hayo yakiendelea.

Moloko bado anatamani kubaki zaidi Tanzania endapo atapata ofa nzuri itakayomshawishi kukubali mkataba.

MASTAA YANGA WALIVYOMTAZAMA AZIZ KI LEO AKIFANYA MAAJABU AFCON…. USAJILI MPYA SIMBA , YANGA WASHTUA…., GAMONDI ASIFIWA…MAKOCHA WATIA NENO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply