Habari za Yanga
Habari za michezo

SIKU MOJA BAADA YA KUPEWA ‘THANK YOU’….KONKONI AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA ALICHOTAKA YANGA….

admin January 17, 2024 6:35 am

Straika Hafiz Konkoni amekiri kufikia makubaliano na Yanga kutolewa kwa mkopo, ambapo kwa sasa amesisitiza anahitaji kwenda nyumbani kwao Ghana, akapumzishe akili yake kidogo.

Amesema atakwenda kucheza soka la kulipwa nchini Cyprus ambako atacheza miezi minne pekee, ingawa hakutaja ni timu gani.

“Sikutaka kuondoka Yanga, ila kwa usalama wa karia yangu imenibidi nifanye maamuzi hayo, nje na hapo ningelazimika kusubiri hadi dirisha kubwa,” amesema na kuongeza;

“Nimepokea ofa nyingi sana kama kutoka Romani na nchi mbalimbali na jambo la msingi zaidi, nitahitaji Yanga inilipe pesa yangu yote ya usajili,”

“Natarajia kuondoka kwenda nyumbani nikapunguze ‘stress’ zilikuwa nyingi sana, baada ya hapo mambo mengine yataendelea,” amesema

DATA ZAKE

Amecheza jumla ya dakika 189 dhidi ya KMC (dakika 26), JKT Tanzania (59), Geita Gold (31), Azam (dakika moja) na Singida Fountain Gate (dakika 72), amefunga bao moja na asisti moja dhidi ya KMC.

USAJILI MPYA SIMBA , YANGA WASHTUA…., GAMONDI ASIFIWA…MAKOCHA WATIA NENO… WAKATI STARS IKITUPA KARATA LEO AFCON….HUYU HAPA MCHEZAJI ALIYEITWA KIUPENDELEO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply