Habari za Yanga leo
Habari za michezo

KONKONI:- TAARIFA ZANGU KUHUSU YANGA ZINA NIA MBAYA….

admin February 7, 2024 6:10 pm

Mshambuliaji wa Yanga SC, ambae ametolea kwa mkopo, Hafiz KonKoni amesema kumekuwa na Habari ambazo sio nzuri kwake na Klabu yake ya kuwa alikuwa anahudumiwa vibaya ndani ya Yanga taarifa ambazo zimesambaa kwa kasi nchini kwao Ghana, amesema sio kweli na zina nia mbaya kwake.

“Natoa shukrani kwa Yanga kwa kunipa nafasi, Yanga ni sehemu ya maisha yangu, na mara zote nilikuwa napokea mshahara wangu kwa wakati na kama ulivyo hizo taarifa sio za kweli.

“Kuhusu hizi habari sifahamu zimetokea wapi watu wanapaswa kujua kuwa nina uhusiano mzuri sana na timu ya Yanga SC, kuanzia Rais wa Klabu, Eng. Hersi hadi mtu wa mwisho kwenye timu, taarifa hizi zimesababisha mvutano kwa familia yangu.

“Nimefurahia maisha hapa na timu yangu ilikuwa inanihudumia vizuri sana, bado niko Tanzania najiandaa kujiunga na timu yangu mpya,” amesema Hafiz Konkoni.

KIGOGO YANGA ALIA MASHABIKI KUDHULUMIWA NA WACHEZAJI….ISHU IKO HIVI… WAKATI DIARRA AKIRUDI TZ KESHO…UKIMYA WA AZIZ KI WAIBUA MASWALI YANGA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply